TANGAZO

Chuo cha Ufundi Arusha kinawatangazia wanafunzi wote wanaopenda kujiunga na kozi za VETA (NVA Level III) kwamba kozi hiyo inatarajiwa kuanza mwanzoni mwa mwezi Julai 2018. Sifa za kujiunga ni kama ifuatavyo:

·         Cheti au matokeo ya level II (VCII)- awe amefaulu masomo yote ya Level II

·         Cheti cha kidato cha nne

·         Cheti cha kuzaliwa

Gharama za masomo ni kama ifuatavyo:

·         Ada kwa mwaka ni shilingi laki nne tu (400,000/-)

·         Gharama za fomu ni shilingi elfu ishirini tu (20,000/-)

·         Gharama za kitambulisho ni shilingi elfu kumi tu (10,000/-)

·          Gharama za usajili ni shilingi elfu tatu (3,000/-)

Jumla kuu ni shilingi laki nne na elfu thelathini na tatu (433,000/-)

Maombi yataanza kupokelewa kuanzia tarehe 20/05/2018 hadi tarehe 06/07/2018

Fomu za maombi zitapatikana Ofisi ya Msajili, Chuo cha Ufundi Arusha

Karibuni sana.