Chuo kinapenda kuwatangazia orodha ya kwanza (Batch 1) ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na mafunzo ya stashahada (ordinary diploma) katika fani mbalimbali za ufundi zinazotolewa na Chuo cha Ufundi Arusha (ATC) kwa mwaka wa masomo 2019/2020. Majina ya wanafunzi waliochaguliwa yatawasilishwa NACTE kwa uhakiki. Wanafunzi waliochaguliwa wanapaswa kufanya UTHIBITISHO wa kukubali kujiunga na kozi aliyochaguliwa kwa kulipa kiasi cha shilingi 50,000/- kabla ya tarehe 16/08/2019. Kiasi hiki cha malipo kitakuwa ni sehemu ya ada kwa mwaka wa masomo 2019/2020 na haitarudishwa (non-refundable) kwa watakaoshindwa kuripoti Chuoni kwa wakati.

Baada ya tarehe 16/08/2019, Chuo kitatoa nafasi husika kwa waombaji wengine walio katika orodha ya kusubiri (waiting list). Majina ya waliothibitisha kujiunga na kozi husika yatawekwa kwenye tovuti ya Chuo tarehe 28/08/2019 sambamba na orodha ya pili (Batch 2).

NB: Kwa wale ambao hawakulipa ada ya maombi (application fee) ya TZS 10,000/- wanaagizwa kufanya hivyo kupitia utaratibu uliopo kwenye tangazo kabla ya kuthibitisha kukubali kujiunga na kozi husika. Kwa yeyote ambaye hatalipa ada ya maombi na ile ya kuthibitisha jina lake litaondolewa kwenye udahili wa Chuo cha Ufundi Arusha.

Namna ya kulipa (mode of payment)

Mwanafunzi aliye chaguliwa anapaswa kutumia namba maalumu ‘CONTROL NUMBER’ ambayo imeambatanishwa na jina lake. Namba hiyo itumike kulipia 50,000/- kwenye tawi lolote la NMB/CRDB au WAKALA wao nchini. NB: Baada ya malipo kufanyika benki, unashauriwa kutunza hati ya kuweka fedha benki (pay in slip) na ufike nayo siku ya kufungua Chuo yaani tarehe 28/10/2019. Maelekezo ya kujiunga (joining instructions) yatatolewa kwa wale waliofanya UTHIBITISHO wa kukubali kujiunga na kozi aliyochaguliwa.

KARIBUNI SANA CHUO CHA UFUNDI ARUSHA, CHUO PEKEE NCHINI KINACHOTOA MAFUNZO YA ELIMU YA UFUNDI YATAKAYOKUWEZESHA KUPATA AJIRA AU KUJIAJIRI