TAARIFA KUHUSU UWEPO WA TUHUMA ZA RUSHWA YA NGONO

 

ARUSHA, AGOSTI 6, 2019

Uongozi wa Chuo cha Ufundi Arusha (ATC) unapenda kutoa taarifa kwa umma wa Watanzania na Wadau mbalimbali wa Elimu na hasa Chuo cha Ufundi Arusha kuwa umepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya kushikiliwa kwa mtumishi wetu na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Arusha, kwa tuhuma za kuomba  Rushwa ya Ngono kwa Mwanafunzi wa Chuo cha Ufundi Arusha  siku ya Ijumaa Tarehe 02 Agosti, 2019.

Uongozi wa Chuo unaahidi kutoa ushirikiano wa aina yoyote kwa vyombo vinavyohusika na uchunguzi wa suala hili ili kutoa haki stahiki kwa pande zote zinazohusika. Chuo cha Ufundi Arusha kama Taasisi ya Umma kinapinga vitendo vyote vibaya visivyoendana na maadili  ya Utumishi wa Umma.

 

Imetolewa na:

 

Gasto Leseiyo

Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano

Chuo cha Ufundi Arusha