ATC STAFF SAVINGS AND CREDIT CO-OPERATIVE SOCIETY

(ATC STAFF SACCOS LTD)

ATC STAFF SACCOS LTD ilisajiliwa rasmi tarehe 8/2/2013 na kupewa Hati Na. AR. 688.

Ofisi za ATC Saccos Ltd zinapatika kwenye bweni namba mbili chumba na. 5 

MADHUMUNI YA KUANZISHWA KWA ATC STAFF SACCOS LTD

 Madhumuni ya kuanzishwa kwa ATC STAFF SACCOS LTD ni kuinua, kuimarisha na kuendeleza hali ya kiuchumi na kijamii ya wanachama wake kwa kufuata Sheria, Kanuni na taratibu za Vyama vya Ushirika. Ili kufanikisha madhumuni haya, ATC SACCOS LTD itafanya yafuatayo:-

a)       Kuhamasisha wanachama wake kujenga tabia ya kujiwekea akiba, Hisa na Amana mara kwa mara;

b)     Kupokea na kutunza Akiba na Amana za wanachama kwa njia rahisi na salama huku ikilipa riba kadri wanachama watakavyokubaliana;

c)     Kutafuta vyanzo vya fedha ili kujenga na kuimarisha mtaji kwa ajili ya kutoa mikopo kwa wanachama kwa masharti na riba nafuu;

d)     Kuwaelimisha wanachama kujijengea tabia ya kukopa kwa busara na kutumia vizuri mikopo kwa ajili ya kuinua hali zao za maisha kiuchumi na kijamii;

e)     Kubuni na kutoa bidhaa mbalimbali za kifedha (Financial products) kwa wanachama ili waweze kushiriki zaidi katika kuimarisha mtaji wa chama na mitaji yao binafsi na kuleta mvuto kwa wasio wanachama kujiunga na chama;

f)      Kuweka kwa usalama fedha za chama na wanachama kwa kuanzisha mipango ya kukabiliana na majanga na/au kuweka bima za fedha zinazofaa;

g)     Kuwashauri wanachama kuandaa mipango yao ya maendeleo katika kuwekeza mitaji kwenye miradi ya kiuchumi na huduma za jamii;

h)     Kutoa elimu kwa wanachama kuhusu dhana ya ushirika na manufaa yake, ujasiriamali na tasnia nyingine zinazohusiana na miradi inayoendeshwa na kutekelezwa na wanachama wake; na

i)       Kufanya mambo mengine ambayo yataimarisha na kuendeleza hali ya uchumi wa chama na wanachama.

 

 

UONGOZI WA ATC ATC STAFF SACCOS LTD

WAJUMBE WA BODI 

               

 Humuri Haymale

Mwenyekiti

                    

Dr. Naisujaki Lyimo

Makamu Mwenyekiti

 

                  

Pascal Jao

Mjumbe

                 

 Frank Moshi

Mjumbe

                   

Judith Mwase

Mjumbe

                

Bahati Kamwela

Mjumbe

                    

Bahati Sule

Mjumbe

 

                      

Neema Sambo

Katibu

 

 

 

 

KAMATI YA USIMAMIZI

                

Juma Heri

                  

Elineema Msuya

                     

Jane Lisah

  

 

KAMATI YA MIKOPO

                

Bahati Sule

 

Jane Lisah

Bahati Kamwela