ATC NA RUWASA ZASAINI MKATABA
Mkuu wa Chuo cha Ufundi Arusha (ATC), Dkt. Musa N. Chacha na Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA), Mhandisi Clement KIVEGALO wakionesha Mkataba wa makubaliano wa Utengenezaji wa Dira za Maji za Malipo ya kabla ya Matumizi baina ya ATC na RUWASA waliosaini leo 21 Juni, 2022, jijini Dodoma na kushuhudiwa na Waziri wa Maji Mhe. Juma Aweso na Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Omary Juma Kipanga (Hayupo kwenye picha). Mkataba huu utakiwezesha Chuo cha Ufundi Arusha Kutengeneza Dira za Maji za Malipo ya Kabla ya Matumizi zipatazo mia moja ambazo zitatumiwa na RUWASA katika kuboresha Makusanyo na matumizi ya maji vijijini kwa kipindi cha miezi sita.