+255-(0)27- 297 0056 Junction of Moshi-Arusha and Nairobi Roads rector@atc.ac.tz SMS Online Application CMU

contact info

+255-(0)27- 297 0056
Junction of Moshi-Arusha and Nairobi Roads
SMS
CMU

Post Details

BILIONI 10 KUJENGA MTAMBO WA KUFUA UMEME CHUO CHA UFUNDI ARUSHA, KAMPASI YA KIKULETWA

Chuo cha Ufundi Arusha (ATC) kiko mbioni kutengeneza mtambo wa kufua umeme (Hydropower Plant) utakaokuwa na uwezo wa kuzalisha Megawati 1.6 za umeme ambao pia utatumika kama nyenzo ya kufundishia kwa vitendo wanafunzi wanaosoma program ya Uhandisi Umeme wa maji. Hayo yamezungumzwa wakati wa utiaji saini kuashiria kuanza ujenzi wa mtambo huo kati ya Chuo cha cha Ufundi Arusha na mkandarasi kutoka kampuni ya China ya HNAC Technology Co. Ltd ambayo itajenga mtambo huo kwa gharama ya shilingi Bilioni 10 za Tanzania. Akizungumza baada ya hafla ya utiaji saini, Mkuu wa Chuo cha Ufundi Arusha Prof. Musa Chacha amesema kwamba ujenzi huo utatumia muda mfupi ili kazi ya uzalishaji umeme na kutoa mafunzo ianze haraka. “Mradi unategemea kuchukua miezi 11 kumalizika, tumefanya ukamilike mapema kwa sababu tunauhitaji sana ili Chuo kianze kufanya kazi mwishoni mwa mwaka huu ikiwezekana, lengo kubwa ni kuandaa hawa vijana mapema katika fani za uzalishaji umeme katika nchi zote za Afrika Mashariki” alisema prof. Chacha. Aidha Prof. Chacha aliongeza kuwa umeme utaozalishwa kwenye kituo hicho utarudi kwenye matumizi ya wananchi wenyewe. “Umeme utakaozalishwa hapa utarudi kuwaangazia wananchi wenyewe katika miji yetu, tutauongeza kwenye gridi ya taifa na watanzania waweze kunufaika”. Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya ukandarasi ya HNAC Technology Co. Ltd Bw. Tader Miao aliyepewa tenda ya ujenzi wa mtambo huo amesema kwamba ujenzi huo utakamilika ndani ya miezi 11 kama ilivyopangwa na kwa viwango vilivyokubalika. Ujenzi wa mtambo huo wa kufua umeme unatekelezwa kupitia mradi wa Afrika Mashariki wa kujenga ujuzi kwa mlingano na uingiliano wa kikanda (EASTRIP) ambao umepata fedha kutoka benki ya dunia. Jumla ya shilingi Bilioni 37 za Tanzania zitajenga mabweni, madarasa na kumbi za mihadhara katika kampasi ya Kikuletwa itakayokua kituo cha Umahiri katika sekta ya nishati jadidifu.

  Feb 01, 2024   |