The United Republic of Tanzania
ARUSHA TECHNICAL COLLEGE
Skills make the difference
Post Details
VIJANA 200 WANUFAIKA NA MAFUNZO YA NISHATI JADIDIFU KUPITIA MRADI WA AJIRA KWA MAENDELEO (E4D) KATIKA CHUO CHA UFUNDI ARUSHA
Vijana 200 kutoka mikoa mbalimbali nchini wamenufaika kwa kupata mafunzo ya nishati jadidifu kwenye upande wa umeme wa nguvu za Jua (Sola) yaliyotolewa na Chuo cha Ufundi Arusha (ATC) kupitia mradi wa mafunzo ya kuwezesha vijana kupata ajira ili kuleta maendeleo (E4D) unaotekelezwa na shirika la Kiufundi la Ujerumani (GIZ). Akizungumza kwenye hafla ya kufunga mradi huo iliyofanyika Chuoni hapo, Afisa Biashara Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Bw. Wilfred Kawa amesema kwamba Mradi huo ulilenga kuhamasisha upatikanaji wa ajira kwa vijana ambapo mpaka sasa wameweza kutengeneza vijana 200. βMradi huu ulilenga Zaidi kuwezesha upatikanaji wa ajira kwa vijana na kinamama hapa nchini kama mnavyofahamu kwamba tatizo la ajira ni tatizo la kidunia, kuanzia mwaka 2020 mpaka sasa tumeweza kutoa mafunzo kwa vijana 200 pamoja na kutengeneza walimu wa kutoa ujuzi wapatao 18 watakaoendelea kutoa mafunzo ya aina hiiβ alisema Bw. Kawa. Naye Kaimu Mratibu wa Mradi huo Mhandisi Dennis Mbangulla ameeleza kwamba βgharama za mradi huu ilikua ni Euro 235,000/- ambazo zimekwenda kwenye kazi mbalimbali ikiwemo Chuo Cha Ufundi Arusha kupitia mitaala ya kufundisha Sola na kuiboresha ifanane na mazingira ya sasaβ. Kwa upande wake mmoja wa wahitimu wa mafunzo hayo Bw. Said Hamza ameupongeza mradi wa E4D na Chuo cha Ufundi Arusha kwa kupatiwa mafunzo hayo na kueleza kuwa kwa sasa yeye pamoja na baadhi ya wahitimu tayari wameajiriwa kwenye kampuni mbalimbali za Sola. Aidha aliomba mradi huo uendelee kufadhili mafunzo hayo kwa awamu nyingine ili watanzania wengi waweze kunufaika.
Other Posts